134 - Tafuta Daima Utakatifu

 134 - Tafuta Daima Utakatifu
"Take Time To Be Holy"

1.

Tafuta daima utakatifu; 
Fanya urafiki na Wakristo tu;
Nena siku zote, na Bwana wako, 
Baraka uombe kwa kila jambo. 

2.

Tafuta daima utakatifu;
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo. 

3.

Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni,
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi. 

4.

Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki, 
Hufanywa tayari kwa kazi yake.

(Amina)

Comments

Popular posts from this blog

121 - Katika Wenye Dhambi

127 - Ni Salama Rohoni Mwangu

126 - Haja Nawe