Posts

Showing posts from April, 2023

121 - Katika Wenye Dhambi

121 - Katika Wenye Dhambi "Chief Of Sinners" 1. Katika wenye dhambi,  Ndimi mkuu wao-  Ila Yesu ukaja,  Kwa dhambi alikufa, Akamimina damu,  Niupate uzima. 2. Ajabu! Pendo lake!  Pendo lililo kuu,  Pendo lisilo mwisho,  Lidumulo milele-  Lililonitafuta  Ingawa sikumpenda 3. Ingawa ni mbaya  Kristo ni vyote kwangu;  Ajua haja zangu;  Huzuni zangu, zake;  Hata katika vita,  Akiwapo Salama.  (Amina)

122 - Yote Namtolea Yesu

 122 - Yote Namtolea Yesu "All To Jesus I Surrender" 1. Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake:  Ninavutwa na upendo, kwa hivyo, najitoa.  Yote kwa yesu, Yote kwa Yesu, Upendo wako hushinda; Yesu, natoa.   2. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake;  Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.  3. Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako;  Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.  4. Yote namtolea Yesu, nami naona sasa,  Furaha ya ukombozi, nasifu jina lake. (Amina)

123.

  (Amina)

124.

  (Amina)

125 - Uniangalie

  125 - Uniangalie "There's Life In A Look 1. Uniangalie atwambia, Yesu aliyetufia; Msalabani ni uzima, Hapa utaipata hazina. Kutazama Kalvari, Kutazama Kalvari,  Ni kupewa kuishi Kuutazama mti wa Kalvari. 2. Ninapojaribiwa ghafula, Shetani hatanitega; Nikitazama msalaba, Nguvu nitaipata kwa Bwana. 3. Msalaba nitautazama Kila wakati daima, Ahadi nitategemea, Hivi kabisa sitaanguka (Amina)

126 - Haja Nawe

 126 - Haja Nawe "I Need Thee Every Hour" 1. Nina haja nawe kila saa; Hawezi mwingine kunifaa. Yesu nakuhitaji vivyo kila saa! Niwezeshe mwokozi, nakujia. 2. Nina haja nawe; Kaa name, Na maonjo haya, hayaumi. 3. Nina haja nawe; kila hali, Maisha ni bure, uli mbali. 4. Nina haja nawe; Nifundishe, Na ahadi zako, zifikishe. 5. Nina haja nawe; Mweza yote, Ni wako kabisa, siku zote. (Amina)

127 - Ni Salama Rohoni Mwangu

127 - Ni Salama Rohoni Mwangu "When Peace Like A River" 1. Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida;  Kwa hali zote umenijulisha ni salama rohoni mwangu. Salama rohoni,   Ni salama rohoni mwangu. 2. Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,  Kristo ameona unyonge mwangu; amekufa kwa roho yangu. 3. Dhambi zangu zote, wala si nusu, huwekwa msalabani;  Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu. 4. Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia:  Utakaposhuka sitaogopa ni salama rohoni mwangu. (Amina)

128 - Taamini Nitii Pia

  128 - Taamini Nitii Pia "When We Walk With The Lord" 1. Namwandama Bwana kwa alilonena, Njia zangu huning`azia; Na nikimridhisha atanidumisha, Taamini nitii pia.  Kuamini, Njiani pweke ni hii  Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii. 2. Giza sina kwangu wala hata wingu,Yeye mara huviondoa; Oga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.  3. Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki. Taamini nitii pia.  4. Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumtoa: Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii, pia.  5. Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia;  Agizo natenda; nikitumwa hwenda, Huamini, nitii pia (Amina)

129 - Kumtegemea Mwokozi

  129 - Kumtegemea Mwokozi "Tis So Sweet To Trust" 1. Kumtengemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa, Kukubali neno lake, Nina raha moyoni. Yesu,Yesu namwamini, Nimemwona thabiti, Yesu,Yesu, yu thamani, Ahadi zake kweli. 2. Kumtengemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kuamini damu yake, Nimeoshwa kamili. 3. Kumtengemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kwake daima napata, uzima na amani. 4. Nafurahi kwa sababu, Nimekutengemea; Yesu,M-pendwa rafiki, uwe nami daima. (Amina)

130 - Yesu Kwetu Ni Rafiki

  130 - Yesu Kwetu Ni Rafiki "What A Friend We Have In Jesus" 1. Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia:  Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia: Lakini twajikosesha,twajitweka vibaya:  Kama tulimwomba Mungu, dua alisikia.  2. Una dhiki na maonjo? Unamashaka pia? Haifai kufa moyo, dua atasikia. Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia:  Atujua tu dhaifu: maombi asikia.  3. Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,  Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.  Watu wakikudharau, wapendao dunia,  Hukwambata mikononi, dua atasikia. (Amina)

131 - Kwa Mahitaji Ya Kesho

  131 - Kwa Mahitaji Ya Kesho "Lord FOr Tomorrow And Its Needs" 1. Kwa mahitaji ya kesho, Sina ombi;  Unilinde nisitende Dhambi leo; Nisiseme neno baya, Mkombozi,  Nisifikiri uovu, Leo hivi.  2. Ningefanya kazi sawa Nakuomba;  Ningekuwa mtu mwema Kila saa;  Mapenzi yako nifanye, Na kutii;  Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi. 3. Kama leo ningekufa Kwa ghafula,  Nitegemee ahadi Zako Bwana. Kwa mahitaji ya kesho Sina ombi;  Uniongeze, nishike Leo hivi. (Amina)

132 - Bwana Ni Mchunga

 132 - Bwana Ni Mchunga "THe Lord Is My Shepherd" 1. Bwana ni Mchunga, Sitahitaji; Majani mabichi malisho yangu. Ananinywesha maji matulivu; Atanirudisha nikipotea.  2. Nipitapo bondeni mwa mauti  U mlinzi wangu sitaogopa; Fimbo lako latosha kunilinda; Ukinifariji sina hasara.  3. Kati ya mateso meza waandaa, Na kikombe changu kinafurika; Umenipaka kichwani mafuta; Nitaulizaje zaidi kwako?  4. Wema na fadhili zinifuate  Siku zangu zote hata milele;  Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana  Katika ufalme wa pendo lake. (Amina)

133 - Popote Na Yesu

 133 - Popote Na Yesu "Anywhere With Jesus" 1. Popote na Yesu nina furaha: Anitumako Yesu ndiyo raha.  Asipokuwako hapanifai,  Akiwapo Yesu, mimi sitishwi. Popote, popote, sina mashaka; Popote na Yesu naweza kwenda. 2. Akiwapo Yesu, si peke yangu;  Na nijapotupwa, akali wangu; Ajaponiongoza njia mbaya, Niwapo na Yesu nashukuria.  3. Akiwapo Yesu naweza lala, Naweza pumzika hata kiyama; Kisha nitakwenda kwake milele,  Akiwapo Yesu furaha tele. (Amina)

134 - Tafuta Daima Utakatifu

 134 - Tafuta Daima Utakatifu "Take Time To Be Holy" 1. Tafuta daima utakatifu;  Fanya urafiki na Wakristo tu; Nena siku zote, na Bwana wako,  Baraka uombe kwa kila jambo.  2. Tafuta daima utakatifu; Uwe peke yako ukimwabudu; Ukimwangalia Mwokozi wako, Utabadilishwa kama alivyo.  3. Tafuta daima utakatifu; Kiongozi wako awe Yesu tu; Katika furaha au huzuni, Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.  4. Tafuta daima utakatifu; Umtawaze Roho moyoni mwako, Akikuongoza katika haki,  Hufanywa tayari kwa kazi yake. (Amina)

135 - Kwa Maombi Nachangamka

  135 - Kwa Maombi Nachangamka "Sweet Hour Of Prayer" 1. Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,  Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu. Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,  Mashaka tumeshinda, wakati wa saa tamu.  2. Saa heri ya maombi, twapeleka dhiki zetu  Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja. Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,  Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.  3. Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia,  Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo. Yesu atatusikia, tutamtafuta daima,  Na tutakapokutana tutamwona - saa tamu! (Amina)

136 - Niwe Kama Yesu

136 - Niwe Kama Yesu "Teach Me Father" 1. Unifundishe, Baba; Ile njia ya sala;  Uniendeshe sana, Niwe kama Yesu. Niwe kama Yesu, Niwe kama Yesu,  Uniongoze, Baba; Niwe kama Yesu, 2. Unipe pendo, Baba, Watu kuwaokoa;  Nyumbani na mjini, Niwe kama Yesu. 3. Na unifahamishe, Wakati ndio mfupi;  Unibidishe, Bwana, Niwe kama Yesu   (Amina)

137 - Saa Heri Ya Sala

  137 - Saa Heri Ya Sala "Tis The Blessed Hour Of Prayer" 1. Saa heri ya sala tunapojidhili, Kama tukija kwake Yesu rafiki; Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi,  Waliochoka sana watapata raha. Saa ya sala, iliyo heri;  Waliochoka sana watapata raha. 2. Saa heri ya sala, ajapo Mwokozi,  Ili awasikie watoto wake. Hutwambia tuweke miguuni pake  Mizigo yetu yote: tutapata raha.  3. Saa heri ya sala, wawezapo kuja Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa;  Moyo wake mpole, atawarehemu;  Waliochoka sana watapata raha. 4. Saa heri ya sala tutakapopewa, Mibaraka ya roho, tukimwamini;  Kwa kuamini kweli hatutaogopa; Waliochoka sana watapata raha. (Amina)

138 - Nitakuandama Kote

  138 - Nitakuandama Kote "I Will Follow Thee" 1. Nitakuandama kote, nitakapoagizwa  Wewe ukiniongoza nami nitaandama. Nitakuandama kote, naam, ulinifia;  Kwa neema yako Bwana napenda kuandama. 2. Njia ijapoparuza kwa miiba na fujo,  Ulitangulia mbele nami nitaandama. 3. Nijapokuta taabu na majaribu kote,  Nakumbuka shida yako, nami nitaandama. 4. Nijapoona ukiwa na mateso makali,  Wewe uliyatikiza nami nitaandama. 5. Ijapo wanipeleka vilindini mwa giza,  Wewe uliyetikiza nami nitaandama. (Amina)

139 - Uniimbie Tena

139 - Uniimbie Tena "Sing Them Over To Me" 1. Uliniimbie tena, Neno la uzima;, Uzuri wake nione, Neno la uzima; Neno hili zuri, lafundisha kweli. Maneno ya uzima ni maneno mazuri Maneno ya uzima ni maneno mazuri 2. Kristo anatupa sote, neon la uzima: Mwenye dhambi asikie, Neno la uzima: Latolewa bure, Tupate wokovu: 3. Neno tamu la injili, Neno la uzima: Lina amani kwa wote, Neno la uzima: Linatutakasa, Kwa haki ya Mwana: (Amina)

140 - Hivi Nilivyo Unitwae

 140 - Hivi Nilivyo Unitwae "Just As I am" 1. Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,  Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, sasa naja. 2. Hivi nilivyo; langu kujiosha roho yangu;  Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja. 3. Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,  Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja. 4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;  Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja. 5. Hivi nilivyo, mimi tu, Siwezi kujiokoa;  Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja. 6. Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;  Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.  (Amina)

141 - Chini Ya Msalaba

 141 - Chini Ya Msalaba "Beneath The Cross Of Jesus" 1. Chini ya msalaba Nataka simama;  Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema; Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,  Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.  2. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;  Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli; Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani. Msalaba umekuwa Ngazi ya mbinguni.  3. Na Yesu Msalabani Walimkemea,  Alikufa niokoke Niliyepotea: Naona ajabu sana Ya mambo mawili  Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.  4. Atakayeonana Na Yesu mbinguni,  Njia yake aanzapo Ni Msalabani; Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana.  Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana. (Amina)

142 - Nasikia Sauti Yako

 142 - Nasikia Sauti Yako "I Hear Thy Welcome Voice" 1. Nasikia mwito, Ni sauti yako;  Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.  Nimesongea mtini pako,  Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.  2. Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;  Ulivyonisfi taka Ni utimilivu.  3. Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,  Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.  4. Napata wokovu, Wema na neema;  Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.  (Amina)

143 - Naamini "Father I Stretch My Hands"

143 - Naamini "Father I Stretch My Hands" 1. Baba sina msaada Ila kwako pekee:  Kama kwangu ungefichwa, Nifanyeje, Baba? Sasa hivi naamini Yesu alikufa, Alimwaga damu yake, Nitoke dhambini. 2. Naamini mwana wako Nipe nguvu zako:  Nijazie mahitaji, Katika saa hii. 3. Ni furaha gani kwangu Kukuona uso!  Nijue sauti yako, Nipate neema. (Amina)

144 - Ni Wako Bwana

144 - Ni Wako Bwana "I Am Thine O Lord" 1. Ni wako, Bwana, ninasikia Unaponena nami;  Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea: Bwana vuta, (vuta) nije nisongee   Sana kwako mtini.  Bwana, vuta, vuta, nije nisongee   Pa damu ya thamani.  2. Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema;  Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama. 3. Nina furaha tele kila saa Nizungumzapo nawe;  Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.   (Amina)

145 - Namtaka Bwana Yesu

145 - Namtaka Bwana Yesu "Take The World" 1. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;  Dunia hunidanganya; Yesu yu mwaminifu. Rehema ni ya ajabu! Pendo bila kipimo!  Wokovu mkamilifu, Amana ya uzima! 2. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;  Kati ya dhoruba kali Yenye wimbo mtamu. 3. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;  Safarini duniani Yeye furaha yangu. 4. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;  Msalaba naamini, Hata namwona Yesu. (Amina)