Posts

121 - Katika Wenye Dhambi

121 - Katika Wenye Dhambi "Chief Of Sinners" 1. Katika wenye dhambi,  Ndimi mkuu wao-  Ila Yesu ukaja,  Kwa dhambi alikufa, Akamimina damu,  Niupate uzima. 2. Ajabu! Pendo lake!  Pendo lililo kuu,  Pendo lisilo mwisho,  Lidumulo milele-  Lililonitafuta  Ingawa sikumpenda 3. Ingawa ni mbaya  Kristo ni vyote kwangu;  Ajua haja zangu;  Huzuni zangu, zake;  Hata katika vita,  Akiwapo Salama.  (Amina)

122 - Yote Namtolea Yesu

 122 - Yote Namtolea Yesu "All To Jesus I Surrender" 1. Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake:  Ninavutwa na upendo, kwa hivyo, najitoa.  Yote kwa yesu, Yote kwa Yesu, Upendo wako hushinda; Yesu, natoa.   2. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake;  Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.  3. Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako;  Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.  4. Yote namtolea Yesu, nami naona sasa,  Furaha ya ukombozi, nasifu jina lake. (Amina)

123.

  (Amina)

124.

  (Amina)

125 - Uniangalie

  125 - Uniangalie "There's Life In A Look 1. Uniangalie atwambia, Yesu aliyetufia; Msalabani ni uzima, Hapa utaipata hazina. Kutazama Kalvari, Kutazama Kalvari,  Ni kupewa kuishi Kuutazama mti wa Kalvari. 2. Ninapojaribiwa ghafula, Shetani hatanitega; Nikitazama msalaba, Nguvu nitaipata kwa Bwana. 3. Msalaba nitautazama Kila wakati daima, Ahadi nitategemea, Hivi kabisa sitaanguka (Amina)

126 - Haja Nawe

 126 - Haja Nawe "I Need Thee Every Hour" 1. Nina haja nawe kila saa; Hawezi mwingine kunifaa. Yesu nakuhitaji vivyo kila saa! Niwezeshe mwokozi, nakujia. 2. Nina haja nawe; Kaa name, Na maonjo haya, hayaumi. 3. Nina haja nawe; kila hali, Maisha ni bure, uli mbali. 4. Nina haja nawe; Nifundishe, Na ahadi zako, zifikishe. 5. Nina haja nawe; Mweza yote, Ni wako kabisa, siku zote. (Amina)

127 - Ni Salama Rohoni Mwangu

127 - Ni Salama Rohoni Mwangu "When Peace Like A River" 1. Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida;  Kwa hali zote umenijulisha ni salama rohoni mwangu. Salama rohoni,   Ni salama rohoni mwangu. 2. Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,  Kristo ameona unyonge mwangu; amekufa kwa roho yangu. 3. Dhambi zangu zote, wala si nusu, huwekwa msalabani;  Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu. 4. Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia:  Utakaposhuka sitaogopa ni salama rohoni mwangu. (Amina)